Maelezo ya Kiongozi Muadhamu kuhusu mauaji ya Waislamu nchini Myanmar
Maelezo ya Kiongozi Muadhamu kuhusu mauaji ya Waislamu nchini Myanmar
Ayatullah Khamenei:

Nchi za Kiislamu zichukue hatua dhidi ya serikali ya Myanmar

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amekosoa kimya na kutochukua hatua jumuiya za kimataifa na wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu kuhusiana na matukio ya maafa yanayojiri Myanmar na kusisitiza kwamba: Njia ya utatuzi wa kadhia hii ni kuchukuliwa hatua za kivitendo na nchi za Kiislamu na kuishinikiza kisiasa na kiuchumi serikali isiyo na huruma ya Myanmar.
Dawa ya matatizo yaliyopo ni kutumia watumishi wenye uwezo
Dawa ya matatizo yaliyopo ni kutumia watumishi wenye uwezo
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo amehutubia hadhara ya makamanda na maafisa wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya (saw) cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, kituo hicho ni mstari wa mbele wa kulinda heshima na nchi.
Kulinda Palestina na kuikomboa ni wajibu halisi wa Kiislamu
Kulinda Palestina na kuikomboa ni wajibu halisi wa Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu ambapo ameashiria siasa za mfumo wa kibeberu za kuzusha mifarakano kati ya Waislamu na kusema kuwa, ni wajibu wa viongozi wa nchi za Kiislamu, wasomi na wanafikra katika ulimwengu wa Kiislamu kuimarisha umoja, kuyazindua mataifa mbalimbali na kusitisha mara moja ...

Anwani nyingine

Zidisheni uwezo wa jeshi ili madhalimu watishike
Husainia ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) mjini Tehran leo (Jumatano) ilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Ali Khamenei ambaye ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran ametembelea maonyesho hayo kwa muda wa zaidi ya masaa mawili na kuona kwa karibu teknolojia za kisasa na za ndani ya Iran za taasisi za elimu za kimsingi ambayo ni matunda ya jitihada, ubunifu, maarifa na utafiti wa wataalamu wa ndani ya nchi na ambayo yana taathira ya moja kwa moja katika kuzidisha uwezo wa kijeshi wa vikosi vya ulinzi vya Iran.
Kiongozi Muadhamu azuru Haram ya Imam Khomeini
Zikiwa zimekaribia siku za Mwenyezi Mungu za Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yanayoanza siku aliporejea kishujaa nchini Iran, Imam Khomeini (MA), Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi amekwenda kufanya ziara katika Haram ya mwanachuoni huyo mkubwa, na sambamba na kumsomea al Fatiha, amemuenzi na kumuombea dua mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kuna udharura wa kupanuliwa zaidi anga ya usomaji vitabu hapa nchini
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Jumapili ametembelea Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran kwa kipindi cha masaa mawili.
Katika shughuli hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, wasimamizi wa vyumba mbalimbali vya maonyesho hayo walitoa maelezo kwa Kiongozi Muadhamu kuhusu vitabu vyao na shughuli za uchapishaji vitabu.