Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Habari

Wizara ya Usalama ni handaki muhimu na jicho la Jamhuri ya Kiislamu
Wizara ya Usalama ni handaki muhimu na jicho la Jamhuri ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo jioni ameonana na Waziri na manaibu na wakurugenzi wa Wizara ya Usalama wa Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, wizara hiyo ni ngao muhimu mno na nyeti na ni jicho linaloangalia mbali na lililomacho la mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Amesisitiza kuwa: Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran ni tabaka lililoundwa na mfumo wa Kiislamu na haipasi kuruhusiwa lipatwe na madhara ya aina yoyote.
Kusahaulika Palestina, lengo kuu la njama za Marekani katika eneo
Kusahaulika Palestina, lengo kuu la njama za Marekani katika eneo
Leo nchana (Jumatano), Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonana na kuzungumza na wakuu wa Mfumo wa Kiislamu na matabaka tofauti ya wananchi ambapo amesema kuwa chanzo halisi cha vita, ukosefu wa usalama na ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu ni madola ya kiistikbari yanayoongozwa na Marekani.
Nasaha 12 muhimu za Kiongozi kuhusu majukumu ya jumuiya za wanachuo
Nasaha 12 muhimu za Kiongozi kuhusu majukumu ya jumuiya za wanachuo
Jumamosi alasiri Julai 2, wanachuo zaidi ya elfu moja wakiwemo wawakilishi wa jumuiya tofauti za wanachuo wamekuwa na mkutano wa kirafiki wa karibu masaa matano na Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambapo wametoa madukuduku yao ya kiutamaduni, kijamii, kisiasa, na kiuchumi kuhusiana na kizazi cha vijana na kupata kusikia mitazamo ya Kiongozi Muadhamu kuhusiana na masuala ya wanachuo, vyuo vikuu, majukumu muhimu ya wanachuo katika mkondo wa mapambano ya taifa na masuala mengine muhimu ya siku.
Wajibu wa Umma wa kutetea Palestina utaonekana Siku ya Kimataifa ya Quds
Wajibu wa Umma wa kutetea Palestina utaonekana Siku ya Kimataifa ya Quds
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo (Jumatano) amekutana na kuhutubia hadhara iliyojumuisha Mkuu wa Idara ya Vyombo vya Mahakama nchini Iran na maafisa na wafanyakazi wa idara hiyo ambako amesisitiza kuwa usafi wa chombo hicho na juhudi za siku zote za kuwaridhisha wananchi ni wadhifa muhimu na lengo kuu la Idara ya Vyombo vya Mahakama. Ameashiria suala la kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa: Kwa Baraka zake Mwenyezi Mungu, siku ya Ijumaa nchini Iran na duniani kote itasikika tena sauti moja ya kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina.
Kulaaniwa uchokozi dhidi ya Sheikh Isa Qassim
Kulaaniwa uchokozi dhidi ya Sheikh Isa Qassim
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu leo alasiri (Jumamosi) amekutana na familia za mashahidi zikiwemo za mashahidi wa tarehe 7 Tir sawa na tarehe 27 Juni na vilevile mashahidi wa kulinda haram takatifu za Watu wa Nyumba ya Mtume (saw).
Watu wafahamishwe hiana ya Marekani kuhusu JCPOA
Katika usiku wa kumkia siku ya kuzaliwa Imam Hassan al-Mujtaba (as), kundi la wanautamaduni, wahadhiri wa mashairi na fasihi ya Kifarsi, washairi vijana na wakongwe nchini pamoja na washairi kadhaa kutoka nchi za Pakistan, India na Afghanistan wamekutana na Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Vyuo vikuu na wanavyuo nawapaswa kuwa wanamapinduzi daima
Vyuo vikuu na wanavyuo nawapaswa kuwa wanamapinduzi daima
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo (Jumamosi) amekutana na wahadhiri wa vyuo vikuu, watu wenye vipaji vya kielimu na watafiti wa vyuo vikuu, vijiji vya sayansi na teknolojia na vituo vya elimu na utafiti ambapo amezungumzia taswira ya malengo ya miaka ishirini ya Mfumo wa Kiislamu kwa ajili ya kufikia kwenye Iran yenye nguvu, izza, huru, yenye kushikamana na dini, tajiri, yenye uadilifu, yenye utawala ya wananchi, safi yenye kupigana jihadi, yenye upendo na wachamungu na kusisitiza kuwa, vyuo vikuu ndiyo msingi na nguzo ya malengo hayo aali.
Maadui wanapanga njama za kuharibu uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu
Maadui wanapanga njama za kuharibu uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo amehutubia hadhara ya viongozi wa mihimili mitatu ya dola, maafisa na wafanyakazi wa Mfumo wa Kiislamu, wakurugenzi wa taasisi mbalimbali na wanaharakati wa masuala ya siasa, jamii na utamaduni akisema kuwa, kuzidishwa uwezo wa nchi kutalinda na kulipa nguvu taifa na nchi. Ameongeza kuwa: Kuweka mipango na kuainisha vipaumbele katika kutatua matatizo mawili muhimu ya mdororo wa kiuchumi na ukosefu wa kazi kutazidisha kasi ya harakati ya kuelekea kwenye uchumi ngangari.
Ayatullah Khamenei awataka wabunge wazingatie uchumi
Ayatullah Khamenei awataka wabunge wazingatie uchumi
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) amekutana na spika pamoja na wabunge wa Majlisi ya 10 ya Ushauri ya Kiislamu ambapo amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa nguvu, hadhi na nafasi ya bunge kuwa kwenye kilele cha mambo yote nchini.
Umapinduzi, njia pekee ya maendeleo na kufikiwa malengo
Umapinduzi, njia pekee ya maendeleo na kufikiwa malengo
Akizungumza leo asubuhi (Ijumaa) mbele ya halaiki kubwa ya matabaka mbalimbali ya wananchi waliofika kuomboleza kwenye Haram ya Imam Khomeini (MA), Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mpainduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa hayati Imam Khomeini (MA) alikuwa mtu muumini, mswalihina na mwanamapinduzi.
Uchumi ngangari na utamaduni wa Kiislamu, vipaumbele vya haraka
Uchumi ngangari na utamaduni wa Kiislamu, vipaumbele vya haraka
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kufunguliwa rasmi duru ya kumi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amewashukuru wananchi kwa kuhudhuria kwa wingi katika uchaguzi wa bunge hilo na kuwataka wabunge wafanye juhudi za kuhakikisha kuwa uchumi ngangari unafikiwa na pia kuchangia kuimarisha na kueneza utamaduni wa Kiislamu nchini.
Kiongozi Muadhamu aonya dhidi ya upenyaji wa adui
Kiongozi Muadhamu aonya dhidi ya upenyaji wa adui
Ayatullahi Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Alkhamisi) ameonana na mkuu pamoja na wajumbe waliochaguliwa na wananchi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mfumo wa Kiislamu na kusema kuwa baraza hilo kwa hakika ni tukio adhimu. Huku akibainisha utambulisho na njia ya kimapinduzi ya baraza hilo, Kiongozi Muadhamu amesisitiza kwamba njia pekee ya kudumu na kuendelea Mfumo na kuthibiti malengo ya Mapinduzi ni nguvu halisi ya nchi na Jihadi kubwa kwa maana ya kutomfuata adui.
Jukumu la wote katika kukabiliana na upenyaji wa adui ni ubainishaji
Jukumu la wote katika kukabiliana na upenyaji wa adui ni ubainishaji
Sambamba na kuwadia tarehe 3 Khordad sawa na tarehe 23 Mei ambayo ni tarehe ya kukumbukwa operesheni ya kifahari ya Beitul Muqaddas ambayo ilipelekea kukombolewa kwa mji wa Khorramshahr, leo asubuhi (Jumatatu) sherehe za kuhitimu masomo ya makadeti wa Chuo Kikuu cha kijeshi cha Imam Hussein (as) zimefanyika katika uwanja wa chuo kikuu hicho na kuhudhuriwa na Ayatullah Ai Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran.
Kiongozi: Suala la maji ya mito ya mpakani linapasa kutatuliwa
Kiongozi: Suala la maji ya mito ya mpakani linapasa kutatuliwa
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo alasiri (Jumatano) ameonana na kuzungumza na Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanistan pamoja na ujumbe anaoandamana nao ambapo amaeashiria masuala mengi ya pamoja ya kiitikadi, kiutamaduni na kihistoria yaliyopo kati ya mataifa mawili haya ya Iran na Afghanistan.
Msingi wa ushirikiano imara na wenye manufaa wa Iran na India
Msingi wa ushirikiano imara na wenye manufaa wa Iran na India
Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo alasiri (Jumatatu) ameonana na Narendra Damodardas Modi Waziri Mkuu wa India ambapo amaeashiria uhusiano mkongwe, wa muda mrefu na wa kihistoria pamoja na mawasiliano ya kiutamaduni na kiuchumi ya watu wa mataifa haya mawili na kusema kuna nyanja nyingi mno za kuimarishwa uhusiano wa pande mbili hizi.

Anwani zilizochaguliwa